WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WANANCHI CUF WACHAPANA MAKONDE HUKO GEITA


KATIKA hali isiyo ya kawaida  baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha wananchi CUF wilayani Geita mkoani Geita  wamechapana makonde  na kupelekea kuahirisha uchaguzi baada ya kutuhumiana kuwepo na mamluki katika ukumbi wa uchaguzi.

Tukio hilo limetokea juzi katika ukumbi wa classic mjini hapa baada ya pande mbili zinazovutana kati ya katibu wa sasa Jovin Mtagwaba na wa zamani Severine Malugu kwa wafuasi wao kutaka mtu wao apite hivyo kupelekea kutuhumiana kuwepo kwa kata ambazo hazina wajumbe halali huku waliopo wakizidi idadi yao.



Katibu wa wilaya Jovin Mtagwaba alipoulizwa kuhusu kutofanyika kwa uchaguzi huo alisema kuwa kilichokuwa kinafanyika ni uhakiki wa wajumbe kwanza ambao unafanywa na msimamizi wa uchaguzi.

Alisema pili ni kusoma taarifa ya chama na tatu kujiuzuru uongozi, kwa hiyo ulipoanza uhakiki baadhi ya kata za Katoma,Nyachiluluma,Nzera na Nkome hazikuwa zimeleta taarifa za uchaguzi wa kata zao wilayani ili tuzitambue na badala yake taarifa walizipeleka taifani.

Naye Seveline Malugu mgombea katibu alisema---

"kuna baadhi ya kata kama za Nzera,Bulela,Kasamwa na Kalangalala hazina wajumbe halali wamepandikizwa tu kwa ajili ya kuharibu uchaguzi kwani kata hizo hazikufanya uchaguzi na hazina wananchama wa kutosha yaani chama huko hakipo sasa hawa wanacham wametoka wapi?’’

Mchuano mkali unadaiwa kuwepo kati ya Jovin Mtagwaba ambaye ndiye kaimu katibu na Severine Malugu  ambaye aliwahi kuwa katibu kabla ya kusimamishwa na kuikaimu nafasi hiyo Jovin ambapo wafuasi wao wamekuwa wakituhumiana kuwepo kwa njama za kudhoofishana kisiasa.

Kwa upande wa msimamizi wa uchaguzi kutoka makao makuu ya chama taifa Yusuph Mbungilo alisema kuwa uchaguzi umeairishwa hadi pale utakapotangazwa tena kutokana na taratibu za kiuchaguzi kutozingatiwa.




.Baadhi ya wanachama wamedai kuwa kumekuwepo na mvutano baina ya pande mbili zinazovutana juu ya uongozi kiasi kwamba kuwepo kwa mamluki ndani ya ukumbi ambapo majina yaliyokuwepo kwenye orodha walikuwa wakiitwa mwanaume anaitika mwanamke jambo lililowafanya kutoamini pande hizi mbili huenda zimeleta mamluki kwenye uchaguzi.

 Na Valence Robert- Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527