TAZAMA PICHA 30- WAREMBO 20 WANAOSHIRIKI SHINDANO LA MISS SHINYANGA MWAKA 2014

Hapa ni katika Hotel ya Diamond Fields mjini Shinyanga-Pichani  ni warembo 20 kutoka maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga wakiwa katika maandalizi ya Shindano la kutafuta Mrembo wa mkoa(Miss Shinyanga mwaka 2014) ambapo Juni 28 mwaka huu,kati ya hao wote atapatikana Miss Shinyanga mwaka 2014.

Washiriki wa kinyang'anyiro hicho wanatoka Kahama,Ushetu,Msalala,Shinyanga vijijini na Shinyanga Senta.Mwandaaji wa mashindano hayo ni Asela Promotions.Kauli mbiu ni "Urembo ,Sanaa na Jamii"

Warembo wakiwa katika pozi,miongoni mwa washiriki katika shindano hilo ni Aisha Ally kutoka Shinyanga Center,Pendo Maxmilian-Shinyanga Center,Jackline Mtaremo-Shinyanga vijijini,Laurencia Mathew-Kahama,Neema Kakimpa-Kahama,Grace Kimaro-Shinyanga Center,Nyangi Warioba-Msalala, Nilamu Abdul-Kishapu,Jackline Jackson-Msalala,Khadija Nyanda-Ushetu,Nicole Sarakikya-Kishapu,Irene Ahmed-Kishapu,Jackline Kimambo-Ushetu,Rose Kibually-Kahama,Rocky Bangili-Kahama,Joyce Ringo-Shinyanga vijijini,Mary Emmanuel-Ushetu,Rukia Samir-Kishapu,Rachel Mushi-Shinyanga vijijini na Sophia Joseph kutoka Msalala.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mwandaaji wa mashindano ya Miss Shinyanga mwaka 2014 Asela Magaka(Pichani) kutoka Asela Promotions amesema washiriki wa kinyang'anyiro hicho cha kusaka mrembo wa mkoa ni 20,na kwamba kabla ya Shindano hilo Juni 28,2014,kutafanyika shindano la kutafuta mrembo mwenye Kipaji mkoa wa Shinyanga(Miss Talent Shinyanga) ambayo yatafanyika Juni 25,2014 katika Ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga huku Mtumbuizaji akiwa ni ISHA MASHAUZI.Warembo hawa 20 watashiriki katika Shindano hili pia ili kujua vipaji mbalimbali walivyonanvyo mbali na urembo wao.
 Asela Magaka amesema kuwa baada ya Miss Talent mkoa wa Shinyanga,shindano la kumpata mrembo wa mkoa wa Shinyanga(MISS SHINYANGA 2014) litafanyika tarehe 28,mwezi huu wa Sita katika ukumbi wa NSSF mjini Kahama ambapo mzee Yusuph,msanii Amani kutoka Kenya na Mo Music watatoa burudani

Warembo wakiwa katika pozi kwenye hoteli ya Diamond Fields mjini Shinyanga ikiwa ni katika maandalizi ya shindano la kumpata mrembo wa mkoa wa Shinyanga mwaka 2014.Matron wao ni Asha Saidi
 Washiriki wa shindano la Miss Shinyanga mwaka 2014 wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Diamond Fields Hotel mjini Shinyanga leo wakijiandaa kwa ajili ya shindano hilo Tarehe 28 mwezi huu katika ukumbi wa NSSF mjini Kahama ambapo Msanii wa nyimbo za Taarabu nchini MZEE YUSUPH,msanii Aman kutoka Kenya na Mo Music  watatoa burudani babu kubwaa siku hiyo mjini Kahama
 Washiriki Miss Shinyanga 2014 wakiwa katika pozi nje ya Hotel ya Diamond Fields mjini Shinyanga mapema leo ambao wote wapo hapo baada ya kuruhusiwa na wazazi wao kushiriki mashindano hayo

Ukiangalia kila mmoja anapendeza kweli kweli na hakuna anayejua nani atabeba taji mwaka huu,ila kitendawili kitateguliwa Juni 28,mwaka huu,na hakika mmoja kati ya 20 pichani ataibuka mshindi



Hawa ni warembo/washiriki wanaowakilisha Kahama wanaowakilisha Kishapu katika shindano la Miss Shinyanga 2014 lililoandaliwa na Asela Promotions ambao wamekuwa wakiandaa mashindano hayo tangu mwaka 1999


Warembo wanaowakilisha Kishapu katika shindano la Miss Shinyanga 2014 lililoandaliwa na Asela Promotions ambao wamekuwa wakiandaa mashindano hayo tangu mwaka 1999

Warembo wanaowakilisha Shinyanga vijijini katika mashindano ya Miss Shinyanga mwaka 2014 yatakayofanyika Juni 28,2014 mjini Kahama 

Washiriki/warembo wanaowakilisha halmashauri ya wilaya ya Ushetu katika mashindano ya Miss Shinyanga mwaka 2014

Washiriki wanaowakilisha Shinyanga Senta katika mashindano ya Miss Shinyanga mwaka 2014

Washiriki wanaowakilisha halmashauri ya wilaya ya Msalala

 Warembo 20 wakipiga saluti nje ya Hoteli ya Diamond Fields mjini Shinyanga leo
 Washiriki wa miss Shinyanga na Miss Talent mkoa wa Shinyanga wakifanya yao leo mjini Shinyanga
 Ni pozi tuuuu
Washiriki wa shindano la Miss Talent na Miss Shinyanga 2014 wakiwa katika pozi

 Washiriki wa Miss talent na Miss Shinyanga wakitembea kwa madaha nje ya Hotel ya Diamond Fields mjini Shinyanga leo
 Duh!! wanatembea kwa pozi haoooo
 Ni Maandalizi tu......ishu nzima Juni 28,2014
 Asikwambie mtu ni vigumu kujua nani ataibuka mshindi,jibu utalipata Juni 28,2014
 Wacha weee
 Haya sasa....
 Hatari kweli kweli......
 Wanaendelea kufanya mambo yao.....
 Picha ya pamoja........
 Wamependeza kweli kweli na kila mmoja anastahili kuibuka kidedeaaa.....
 Daaah....
Warembo hawa 20 wanawakilisha Kishapu,Kahama,Ushetu,Shinyanga Senta na Shinyanga vijijini katika katika Mashindano mawili yaani Miss Tarent Shinyanga litakalofanyika Juni 25,2014 mjini Shinyanga katika ukumbi wa NSSF ambapo Isha Mashauzi atapiga show babu Kubwa na Shindano la Miss Shinyanga litakalofanyika Juni 28,2014 mjini Kahama ambapo mzee wa kazi Mzee Yusuph akiwa na wasanii kibao atafanya makubwa.Mashindano hayo yamendaliwa na ASELA PROMOTIONS.

Asela Promotions wamejizolea umaarufu hapa nchini kwa kazi yao nzuri katika kuandaa mashindano ya kupata mamiss katika mkoa wa Shinyanga na taifa kwa ujumla.

Ikumbukwe kuwa Asela Promotions wameanza kuandaa mashindano ya miss Shinyanga tangu mwaka 1999 na mwaka jana wamepewa Tuzo ya mwandaaji bora wa mashindano ya mamiss Tanzania na sasa dhamira yao ni kupata mrembo atayeshinda kitaifa(atakayeshinda nafasi ya Miss Tanzania kutoka Shinyanga) baada ya miaka mingi kuishia nafasi hadi ya pili mfano,mwaka 2000 mshindi wa pili miss Tanzania alikuwa Lilian Kusekwa kutoka Shinyanga,mwaka 2003 nafasi ya 2 alikuwa Dotto Nusu Lupia kutoka Shinyanga,2005 nafasi ya pili Jenifa John kutoka Shinyanga,2007 nafasi ya tatu miss Tanzania alikuwa Helga Tarimo kutoka Shinyanga na mwaka 2011 nafasi ya 2 ilichukuliwa na Trace Mabula kutoka Shinyanga ambao wote waliandaliwa na Asela Promotions

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog-Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post