Hot News!! SAKATA LA MGONJWA KUOZA MAKALIO NA KUTIMULIWA BUGANDO,MGANGA ANAYEMTIBU AFICHUA SIRI NZITO


Mgonjwa Luhogola katikati(tumeficha picha kwa maksudi) akiendelea vizuri  na matibabu,kushoto ni mganga wa asili anayemtibu

Hali halisi ya makalio ya Joseph Luhogola (38),mkazi wa Kitongoji cha Nyabugera,Kijiji cha Mganza Wilaya ya Chato katika Mkoa wa Geita baada ya Kufikishwa nyumbani kwa mganga wa tiba za asili Chasama

Joseph Luhogola (38),mkazi wa Kitongoji cha Nyabugera,Kijiji cha Mganza Wilaya ya Chato katika Mkoa wa Geita akiwa amelala nyumbani kwa mganga wa tiba za asili Paul Chasama baada ya kutoka hospitali ya Bugando
Kulia ni Mganga chasama akitibu mtoto aliyekuwa amevunjika mguu kuanzia pajani mtoto huyo alishapona,kushoto ni mama wa mtoto na katikati ni bibi wa mtoto

Mganga Chasama kulia akiwa katika picha ya pamoja na mgonjwa aliyevaa jezi kiatikati baada ya kumtibu na kupona

kulia ni Mganga chasama akiwa na mgonjwa aliyewahi kumtibu mguu uliovunjikia kwenye kiwiko-Picha zote na Victor Bariety wa malunde1 blog-Geita.
TIBA za asili zilianza kutumika tangu enzi za mababu zetu, lakini zilikuja kupoteza umaarufu wake baada ya kuingia kwa wakoloni walioleta dawa.

Pamoja na matumizi ya dawa asili kupungua baada ya ujio wa wakoloni, siku za karibuni muamko wa Watanzania kurudi katika dawa hizo umeanza kuongezeka huku ikielezwa kwamba imechangiwa na madhara wanayoyapata watu wanapotumia baadhi ya dawa za hospitali.

Hivi karibuni, mmoja wa matabibu wa tiba hizo za asili,Paul Chasama Luswigilo (52), alifanya mahojiano na mwandishi wa malunde1 blog Victor Bariety na kuzungumzia jinsi anavyowasaidia watu mbalimbali akitumia utaalamu huo aliorithi kwa marehemu baba yake Chasama Luswigilo.

Tofauti na matabibu wengine, Chasama anasema amejikita zaidi kutoa tiba za mifupa ambapo huwa anatumia picha zinazopigwa  hospitali (x-ray) kabla hajamtibu mgonjwa.

Miongoni mwa wagonjwa ambao amekuwa akiwahudumia kwa wingi ni waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda ambao hujeruhiwa wakiwa kazini.

Majeruhi hao wa pikipiki wamekuwa wakiongezeka kila kukicha na kufikia hata kupoteza maisha tangu usafiri huo uliporuhusiwa na serikali kutumika.

“Kwa kweli huwa nikienda pale wodini katika hospitali ya Wilaya ya Geita,na kukuta wagonjwa wakigalagala na kusikilizia maumivu nasikitika sana’’

“Hii yote ni kwa kuwa wanadhani tiba inapatikana tu hospitali bila kujua kuna wataalamu kama sisi tunaoweza kuwaondolea maumivu hayo, tena kwa wepesi,” anasema.

Katika dawa zake hizo kwa wale waliopata ajali na majeraha yao kuonekana kuvilia damu, huwa na dawa maalumu ambayo humwekea mgonjwa na kuyeyusha damu hiyo.

Wakati kwa upande wa wagonjwa waliowekewa vyuma, kuna dawa ya kupaka ambayo husaidia kupunguza maumivu na uvimbe unaokuwepo kati ya chuma na ngozi.

Anasema kwa wajawazito ambao wamekuwa wakifanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua, ana dawa yao ya kuwaepusha kuwa na kovu kubwa la mshono pindi wanapopona na ya kuwaondolea maumivu ya mgongo na kiuno yanayowatokea mara kwa mara.

Tatizo jingine analotibu mtabibu huyu ni la watoto kushindwa kukaza shingo, hasa wanapofikia hatua ya kukaa na wale waliozaliwa na ulemavu wa viungo ambao anasema kutokana na mifupa yao bado kuwa michanga ni rahisi kuwatibu.

Wakati akiwa na tiba hizo, Chasama anaumia sana kuona kwamba haziwezi kutumika hospitali kama tiba mbadala kwani anapofika maeneo hayo anatamani awaambie madaktari, lakini kutokana na sheria za kitabibu inashindikana.

Kutokana na hali hiyo alitaka kuwepo na utaratibu wa kubadilishana wagonjwa kati ya watabibu wa tiba asili na hospitali, anaosema umefanikiwa kwa kiasi kikubwa nchini China.

Katika harakati za kufikia huko, anasema anao mpango wa kupeleka dawa zake kwa mkemia mkuu ili kwenda kuthibitishwa ubora wake, na pia ana mpango wa kuzungumza na Hospitali mbalimbali zenye vitengo vya  viungo ili kutumia dawa zake ikiwemo ile ya kuweka ndani ya P.O.P na kumsaidia mgonjwa kubaki na maumbile yake kwani wengine hujikuta wakivimba au wakibadilika rangi eneo wanalofungwa bendeji hiyo ngumu.

Chasama amekuwa na changamoto mbalimbali anazokabiliana nazo katika kufanya kazi zake ikiwemo ukosefu wa mashine ya kumwezesha kusaga dawa hadi kufikia hatua ya poda kwa madai kwamba nazo ni ngumu kutengeneza kama ilivyo mifupa.

Anasema mashine hiyo inatumia nguvu za umeme zenye watt 1000, wakati kwa sasa kutokana na kutokuwa na uwezo anatumia kifaa aina ya blender na kutwanga kwa kutumia kinu kisha kupitisha kwenye chekecheo.

Wito wake kwa jamii ni kuwa na imani na dawa zao, kwa kuwa wengi wao mbali na kutomaliza dozi kama wanavyotakiwa, wamekuwa wa kwanza kuuliza kama kweli watapona, maswali ambayo anadai si rahisi kuulizwa daktari wa hospitali.

Pia amewataka kuhakikisaha wanayalinda mazingira ili kuweza kuhifadhi dawa za asili ambazo nyingi zinapatikana katika misitu ya asili.

Anaitaka serikali kujenga utaratibu wa kubadilishana wagonjwa kwa kuwa magonjwa mengine hayatibiki hospitali, huku akitolea mfano kwamba huwa anapata wagonjwa madaktari ofisini kwake.

Kuhusu kiwango chake cha elimu, anasema mbali na elimu yake ya msingi aliyonayo,marehemu baba yake alimfundisha masuala ya huduma ya kwanza, hivyo anajua vema kumhudumia mgonjwa atakayefika kwake akiwa mahututi.

Chasama anasema amekuwa akitoa huduma hata kwa wakazi wa mikoani bila hata ya kuja kwani zaidi atahitaji picha zao na kama ni dawa anawatumia kwa njia yoyote ambayo itakuwa rahisi kwao.
JAMHURI lilifanya mahojiano na baadhi ya wagonjwa waliotibiwa na Chasama , akiwemo Mwesi anayedai alivunjika mguu baada ya kupata ajali ya gari alipokuwa kwenye kazi yake ya utingo akitokea Kahama kuja Geita.
Anasema ilikuwa mwaka 2010 alipopatwa na ajali hiyo, lakini baada ya kwenda hospitali alielezwa anapaswa kukatwa mguu wake.
Kutokana na hali hiyo aliwaeleza ndugu zake watafute njia mbadala ya kunusuru mguu wake huo usikatwe.
Anasema wakati akiwa katika kujiuguza huko ndipo alipompata ndugu yake mmoja aliyewahi kutumia dawa za Chasama, ambaye alimpeleka na tangu alipotumia dawa hizo ndani ya mwezi mmoja alipona mguu wake ambao uliunga kabisa na anaendelea na kazi zake za utingo kana kwamba hakuwahi kupata ajali na kuvunjika mguu.
Mgonjwa mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Rameck anasema alipata ajali mwanzoni mwa mwaka  2013 akiwa kwenye machimbo ya dhahabu huko Nyarugusu na kuvunjika mguu kwenye viwiko. Alikwenda hospitali na kufungwa P.O.P, lakini bado mguu huo ukaendelea kumuuma.
Anasema alipofika kwa Chasama baada ya kupelekwa na rafiki yake, alipatiwa tiba na hadi sasa alikwisha sahau kama amewahi kuvunjika mguu.
Wengi wanaweza kujiuliza huyu tabibu ni nani?Paul Chasama Lushwigilo si  geni masikioni mwa watu wengi ndani na nje ya nchi hususani wale wanaofuatilia vyombo vya habari,hususani magazeti na mitandao ya kijamii.

Jina lake limeanza kuvuma hivi karibuni kwenye vyombo vya habari mara baada ya kumpokea na kuanza kumtibu mgonjwa aliyepooza mwili wake kuanzia kifuani hadi miguuni na kuoza makalio yake kisha kutimuliwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando alikokuwa amelazwa baada ya kupata ajali hivi karibuni.

Mgonjwa huyo,Joseph Luhogola(38),mkazi wa kitongoji cha Nyabugera,Kijiji cha Mganza Wilayani chato katika Mkoa wa Geita,alipokelewa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Aprili 22 mwaka huu akitokea katika hospitali ya Wilaya ya Chato muda mfupi baada ya kupata ajali na alitimliwa hospitalini hapo Mei 27 mwaka huu.

Haijajulikana hadi sasa kisa cha wauguzi na madaktari wa Bugando kumtimua mgonjwa huyo katika hali hiyo ambayo hata hivyo ilitokana na uzembe wao wenyewe.

Alipotafutwa Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Dk Charles Majinge naye hakuwa na majibu ya kuridhisha ambapo alisema hajui kama hicho kidonda kilisababishwa na ajali au la,na kueleza kwamba inawezekana kule kulala kwa muda mrefu kutokana na kupooza huko alitengeneza kidonda.

 “Ili kuweza kueleza haya Mgonjwa aje Tuone,Tutafute jarada lake tuweze..kufuatilia ni nini kilitokea na sio kawaida mtu kumruhusu akiwa na kidonda kikubwa kama unavyokielezea,”alisema majinge na kuongeza.

“Labda walimweleza mgonjwa hawakuwaeleza ndugu na ndiyo maana hawakujua kama ana hali hiyo,sasa mwambie aje na nyaraka za Taarifa zake.Lakini kuna tatizo la watu kama hao wamekuwa wakiomba ruhusa ya kuagwa ili waende kwa waganga wa kienyeji hasa hao wenye kupooza mwili’’.

Alifafanua kwamba”Siwezi kusema kama hakuna kidonda na kwa tatizo hilo kulingana na Vitanda vyetu,Tatizo la kuendeleza kidonda lipo,Na wengi wanaokuja hapa wanaomba kuruhusiwa ili kwenda kwa waganga wa kienyeji”

Wakati Dk Majinge anadai hivyo,mgonjwa Luhogola(38),anadai alifikishwa Bugando akiwa na majeraha sehemu za kichwani na yalipona kwa muda mfupi,na kwamba matatizo mengine kama kupooza na kuoza makalio hakuwahi kuwa nayo na kwamba kauli yake inalenga kujitetea mbele ya wakubwa zake na kwa watanzania ambao wameguswa na ugonjwa wake.

Hata hivyo baadhi ya watu walioguswa na kituko hicho,mbali na kusikitishwa na tukio hilo wao walimtaka mwandishi wa habari hizi kutoa mawasiliano ya Mtaalamu wa tiba za asili upande wa mifupa aliyejitoa mhanga kuokoa maisha ya kijana Luhogola almaarufu Mtoto wa Bugando.

Lengo la wasomaji si jingine bali walidai tukio hilo limewashitua sana hivyo na kwamba kuna wagonjwa wengi ambao wanasumbuliwa na matatizo kama hao na wamekuwa wakifia mahospitalini kwa kukosa msaada wa wataalamu na kwamba iwapo namba zake zikiwekwa wazi yawezekana ataokoa roho za watanzania wengi.
Huyu ndiye Paul Chasama

Paul Chasama,alizaliwa 1962 katika kitongoji cha Bulima,Kijiji cha Nyabusalu Wilaya ya Misungwi Mkoani  Mwanza.

Chasama ambaye ni mtaalamu wa tiba za jadi kwa kuunga mifupa na kurudisha viungo vya mwili vilivyochengana alianza kutibu mifupa iliyovunjika na watu waliopooza mwili Tangu mwaka 1997 alipoanza kutoa tiba hiyo na kwamba utalaamu huo aliupata kutoka kwa wazazi wake.

Wakati Chasama anaanza kazi hiyo alikuwa katika kijiji cha Nyarugusu Wilayani Geita Mkoani Mwanza.

Akimzungumzia Mgonjwa huyo,Chasama anatamba kuwa anao uhakika wa kupona ugonjwa unaomsumbua(wa kupooza) na kwamba watanzania wakae mkao wa kula kumuona mwenzao akiwa anadunda mtaani kwani tatizo kubwa ni kidonda ambacho alidai nacho kitatoweka na kubaki historia.

Anasema“Walichokosea huko Hospitalini ni kule kumlaza chali kila siku bila kumgeuza hali iliyosababisha kuwa na kidonda kama hicho.Lakini suala la Kupooza halitachukua Muda mrefu na hata hiki kidonda kitayeyuka na watanzania hawataamini kitakachotokea”

Nakwambia hivi ndugu mwandishi,mimi ndiye Chasama kama umewahi kumsikia ninachokueleza ndugu mwandishi huyu mgonjwa nitamponya na kama kuna mtu haamini asubili aone,nimeshakutana na kesi kubwa na huyu hapa naweza kusema haumwi lakini niliwaponya na sasa ukiwaona huwezi amini kama waliwahi kuumwa.

AINA YA WAGONJWA ANAOWAPOKEA

Anasema amekuwa akipata wagonjwa wenye matatizo kama hayo pamoja na wale waliovunjika mifupa,kuhama viungo na kuvunjika miguu lakini wamekuwa wakipona kwa kutumia miti shamba.

Hata hivyo alifichua siri kubwa baada ya kudai kubwa asilimia kubwa ya wagonjwa anaowapokea ni wale ambao tiba za hospitalini zinakuwa zimeshindwa kufanya kazi.

Aliwataka watu wenye wagonjwa wanaosumbuliwa na uti wa mgongo,viungo vya mwili vilivyochengana,vidonda vya tumbo na kupooza wafike haraka katika kitongoji cha Mwenge,Kijiji cha Nyankumbu Wilayani Geita ili wapate huduma hizo.

Alidai kuwa,kumekuwepo na desturi kwenye baadhi ya hospitali zetu za kuwakata miguu watu wanaopata ajali za magari na pikipiki jambo alilodai hawatendewi haki na kuwaomba wenye matatizo kama hayo kufika mara moja ofisini kwake Nyankumbu Geita.

‘’Kuna watu wamekuwa wakipata ajali na kuvunjika miguu,na wanapofikishwa hospitalini miguu hiyo humaliziwa kwa kukatwa,hii siyo halali hata kidogo na mimi nipo kwa ajili ya kazi ya kuponya watun kama hao,hata kama kuna mtu aliyesagwa mifupa yake ikawa unga mimi ninao uwezo wa kuirejesha katika hali yake ya awali.

Chasama amesema iwapo atapatiwa msaada na wasamalia wema atatimiza malengo yake kwa kufungua CLINIC kubwa ya kutibu magonjwa yote ambayo anao utaalamu wake.

Aidha Chasama aliiomba serikali kuwathamini wataaalamu kama na ikibidi iangalie uwezekano wa kuwachukua wataalamu wote wanaorudisha viungo vya mwili vilivyochengana na kuwaweka kwenye hospitali zetu ili wasaidiane na madaktari kuokoa roho za watanzania.

WALIOTIBIWA NA CHASAMA WANENA

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi baadhi ya watu ambao walikuwa na matatizo kama ya Luhogola na sasa walikwishapona,waliwataka watanzania wenye matatizo kama hao kukimbilia kwa Chasama kuokoa roho zao.

Walisema,Chasama anastahili pongezi kwa kile walichodai mbali na kuwa na tiba za uhakika hatozi kiwango kikubwa cha pesa na anachojali ni utu.

‘’Huyu Chasama ni wa kupongezwa maana kama unatatizo hakimbilii pesa yako bali anakutibu na ukishapona ndiyo anakuchaji pesa kidogo tofauti na waganga wengine’’alisema  Mwesi aliyewahi kuvunjika paja baada ya kupata ajali na aliyemponya ni Chasama.

Bw,Mayengo Mayengo,aliyewahi kuwa na tatizo la kuhama kwa nyonga,Rameck Rameck aliyevunjika mguu sehemu ya kiwiko wamedai kuwa hakika bila Chasama hawajui kwa sasa hali zao kimaisha zingekuwaje na wanamshukuru kwa kuwaponya maana mpaka sasa wanaendelea kupiga mzigo na kujiingizia kipato.

Baadhi ya mawasiliano ya simu ya watu ambao wamewahi kutibiwa na kupona ni pamoja na Mama Shabani 0686739829,Rameck 0789937517,Mayengo 0756822690,na Eliud 0785418686 iwapo huamini unaweza kuuliza kwa hawa ambao wamewahi kunufaika na huduma ya Chasama.

KAMA KUNA MTU ANA TATIZO AWASILIANE NA MTAALAMU WA KUUNGA MIFUPA CHASAMA KWA SIMU 0787469670

Na Victor Bariety-Malunde1 blog Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527