Mgeni rasmi
katika warsha hiyo,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Anna rose Nyamubi,ambaye ni mdau
wa maendeleo na mwanafamilia wa Umoja wa Mataifa(siku za nyuma aliwahi kufanya
kazi na Umoja wa mataifa katika shirika la UNICEF),alisema nchi ya Tanzania
inatekeleza malengo ya millenia kupitia ilani ya ccm katika kuwaletea maendeleo
wananchi wake hususani katika kupunguza umaskini.Katika hatua nyingine Nyamubi aliwataka vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na Umoja wa mataifa.Mkuu huyo wa wilaya aliongeza
kuwa serikali inawajali vijana hivyo kuwataka kusoma kwa malengo kwani bila
elimu dunia itawaacha na kuwataka kuacha kutegemea wazazi wao kwamba watarithi
mali.Aidha Nyamubi alitumia fursa hiyo kuwataka wazazi ambao hawajapeleka
watoto wao kidato cha kwanza wawapeke haraka kabla ya kuwachukulia hatua.
|
Awali katika
shule ya sekondari Chamaguha katika manispaa ya Shinyanga,ambako maafisa wa
Umoja wa Mataifa walifanya ziara yao, Mkutubi kutoka kitengo cha habari Umoja
wa Mataifa nchini Tanzania bi Harriet Macha akizungumza na wanafunzi wa shule
hiyo ambao wamedhamiria kuanzisha klabu ya Umoja wa Mataifa katika shule hiyo
ambayo itaundwa na wanafunzi kuanzia 10 na kuendelea.Hapo anaonesha vitabu na
vipeperushi mbalimbali vinavyohusu umoja wa mataifa ambao ulianzishwa mwaka
1945 baada ya vita ya pili ya dunia.Hivi sasa umoja wa mataifa una nchi
wanachama 193 duniani kote na nchi 3 pekee siyo nchi wanachama wa Umoja
huo,nchi hizo ni Taiwan,Cossovo na Vatican
|
Ni katika
ofisi ya walimu katika shule ya sekondari Chamaguha katika manispaa ya
Shinyanga,muda mchache tu baada ya maafisa kutoka Umoja wa mataifa kuwasili
katika shule hiyo kabla ya kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo.Aliyesimama ni
kaimu mkuu wa shule hiyo bwana Malongo Maganga akiwakaribisha wageni hao ambapo
aliupongeza Umoja wa Mataifa kwa kuwafikia na kufurahishwa na mpango wake
kuhusu elimu ya uzazi wa mpango kwa wanafunzi kwani itawasaidia kuongeza uelewa
na kujilinda zaidi ili kutimiza malengo yao.Alisema jamii inaamini kuwa elimu
hiyo ni kwa ajili ya akina mama pekee.Aidha mwalimu Maganga alisema tayari
shule yake imefungua faili kwa ajili ya klabu ya Umoja wa Mataifa kwa wanafunzi
wa shule hiyo
|
Social Plugin